• HABARI MPYA

  Friday, April 23, 2021

  MESSI APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA GETAFE 5-2 LA LIGA

  MUARGENTINA Lionel Messi jana amefunga mabao mawili, Barcelona ikiibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Getafe kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa Camp Nou.
  Messi alifunga mabao yake dakika ya nane na 33, wakati mabao mengine ya kikosi cha Ronald Koeman yalifungwa na Sofian Chakla aliyejifunga dakika ya 38, Ronald Araujo dakika ya 87 na Antoine Griezmann kwa penalti dakika ya 90 na ushei.
  Mabao ya Getafe yalifungwa na Clement Lenglet aliyejifunga dakika ya 12 na Enes Unal dakika ya 69 na sasa Barcelona inafikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 31 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi mbili na Real Madrid na pointi tano na Atletico Madrid ambao wamecheza mechi 32 kila mmoja.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA GETAFE 5-2 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top