• HABARI MPYA

  Wednesday, April 21, 2021

  MIQUISSONE NA MUGALU WAFUNGA KAITABA SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 BUKOBA

   

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwahapa wenyeji, Kagera Sugar mabao 2-0 jioni ya leo katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 13 na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu dakika ya 24.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 23, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na watani wao, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIQUISSONE NA MUGALU WAFUNGA KAITABA SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top