• HABARI MPYA

  Monday, April 26, 2021

  BIASHARA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 NA POLISI TANZANIA NAYO YAIPIGA MTIBWA PALE PALE MOROGORO

  TIMU ya Biashara United imezinduka na kuichapa Kagera Sugar 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Mabao ya Biashara United yamefungwa na Deogratius Mafie dakika ya 24 na Lenny Kisu dakika ya 28, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 84.
  Kwa ushindi huo, Biashara United imefikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 28 ingawa inabaki nafasi ya nne, ikiizidi pointi nne KMC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 27 za mechi 28 ikiangukia nafasi ya 16.


  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imewachapa wenyeji Mtibwa Sugar 2-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mabao ya Polisi yamefungwa na Abdulaziz Makame dakika ya 33 na Tafiq Seif dakika ya 40, wakati la Mtibwa limefungwa na Kelvin Sabato dakika ya 51.
  Polisi Tanzania inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 28 na kusogea nafasi ya nane, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 28 za mechi 27 katika nafasi ya 14 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 NA POLISI TANZANIA NAYO YAIPIGA MTIBWA PALE PALE MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top