• HABARI MPYA

  Friday, April 23, 2021

  MANCHESTER CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA LIGI KUU YA ENGLAND

  TIMU ya Manchester City imezidi kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Aston Villa juzi Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Wenyeji walitangulia kwa bao la John McGinn dakika ya kwanza tu, kabla ya Phil Foden kuisawazishia Man City dakika ya 22 na Rodri kufunga la ushindi dakika ya 40, wote wakimalizia kazi nzuri za Bernardo Silva.
  Timu zote zilimaliza pungufu baada ya wachezaji wao, beki John Stones wa Manchester City kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 44 na kiungo wa Aston Villa, Matty Cash kutolewa kwa kadi nyekundu pia dakika ya 54 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Ushindi huo unaifanya timu ya kocha Pep Guardiola imefikisha pointi 77 baada ya kucheza mechi 33 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya mahasimu wao wa Jiji, Manchester United ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA LIGI KUU YA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top