• HABARI MPYA

  Friday, April 16, 2021

  AZAM FC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI, KMC YAITANDIKA GWAMBINA FC 3-0 DAR


  BAO pekee la Ayoub Lyanga dakika ya 21 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ya kocha Mzambia, George Lwandamina ifikishe pointi 50 baada ya kucheza mechi 26 na kurejea nafasi ya pili sasa ikizidiwa pointi moja na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imeitandika Gwambina FC 3-0, mabao ya Charles Ilamfya dakika ya 51, Emmanuel Mbuyekure dakika ya 62 na Ally Ramadhani dakika ya 72.
  Kwa ushindi huo, KMC ya kocha mkongwe, John Simkoko inafikisha pointi 39 baada ya kucheza mechi 26 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Biashara United ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.
  Kwa kufungwa leo, JKT inabaki na pointi zake 27 za mechi 26 katika nafasi ya 13 na Gwambina inabaki na pointi 30 za mechi 24 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI, KMC YAITANDIKA GWAMBINA FC 3-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top