• HABARI MPYA

  Thursday, April 08, 2021

  MBAPPE APIGA MBILI PSG YAILAZA BAYERN MUNICH 3-2 UJERUMANI


  TIMU ya Paris Saint-Germain imetanguliza mguu mmoja Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji na mabingwa watetezi, Bayern Munich katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano hiyo usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani.
  Mabao ya PSG ya Ufaransa yalifungwa na Kylian Mbappe mawili dakika ya tatu na 68 na Marquinhos dakika ya 28, wakati ya mabingwa wa dunia yalifungwa na washambuliaji Mcameroon Jean-Eric Maxim Choupo-Moting dakika ya 37 na mkongwe wa Ujerumani, Thomas Muller dakika ya 60.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 13 Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Manchester City na Borussia Dortmund. Man City ilishinda 2-1 juzi England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAPPE APIGA MBILI PSG YAILAZA BAYERN MUNICH 3-2 UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top