• HABARI MPYA

  Tuesday, April 06, 2021

  YANGA SC WAICHAPA AFRICAN LYON 3-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO KIGAMBONI


  TIMU ya Yanga SC leo imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya African Lyon ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Avic Centre, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong, kiungo Mrundi Abdulrazak Fiston na beki mzawa Paul Godfrey 'Boxer'.
  Kocha Juma Mwambusi ameutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya Ligi Kuu dhidi ya KMC Ijumaa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAICHAPA AFRICAN LYON 3-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top