• HABARI MPYA

  Thursday, April 29, 2021

  AZAM FC NA BIASHARA UNITED ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUZITOA POLISI TANZANIA NA RUVU SHOOTING LEO

  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) yote yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika za 25 na 65, wakati la Polisi limefungwa na Marcel Boniventura Kaheza dakika ya 76 kwa penalti.
  Mechi nyingine ya 16 Bora ya ASFC leo wenyeji, Biashara United wameitoa Ruvu Shooting kwa penalti 4-1 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Azam na Biashara zinaungana na Rhino Rangers ya Tabora kutinga Nane Bora ambayo jana iliitoa Arusha FC kwa kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC NA BIASHARA UNITED ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUZITOA POLISI TANZANIA NA RUVU SHOOTING LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top