• HABARI MPYA

  Saturday, April 10, 2021

  YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA KMC MECHI YA LIGI KUU LEO DAR  VINARA, Yanga SC wameendelea kushusha matumaini ya ubingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar sa Salam.
  KMC walitangulia kwa bao la Bryson David dakika ya 29, kabla ya Mburkina Fasso, Yacouba Sogne kuisawazishia Yanga SC dakika ya 46.
  Kwa matokeo hayo, Yanga SC inafikisha pointi 51 baada ya kucheza mechi 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.
  Mabingwa watetezi, Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 tu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Dodoma Jiji FC imewachapa wenyeji, Tanzania Prisons 1-0, bao pekee la Dickson Ambundo dakika ya 55 Uwanja wa Samora, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Nayo Gwambina FC imeitandika Coastal Union 4-0, mabao ya Meshack Abraham dakika ya tisa, Paul Nonga dakika ya 31, Rajab Athumani dakika ya 37 na Jimson Mwanuke dakika ya 75 Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA KMC MECHI YA LIGI KUU LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top