• HABARI MPYA

  Sunday, April 18, 2021

  NKETIAH AISAWAZISHIA ARSENAL DAKIKA YA MWISHO 1-1 NA FULHAM

   

  TIMU ya Arsenal imelazimishwa sare ya 1-1 na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mshambuliaji kinda wa miaka 22, Mnigeria Josh Maja alianza kuifungia Fulham dakika ya 59, kabla ya kinda wa miaka 21 wa England, Edward Nketiah kuisawazishia Arsenal dakika ya 90 na ushei.
  Kwa sare hiyo Arsenal inafikisha pointi 46 baada ya kucheza 32 katika nafasi ya tisa, wakati Fulham imefikisha pointi 27 ndani ya mechi 33 katika nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NKETIAH AISAWAZISHIA ARSENAL DAKIKA YA MWISHO 1-1 NA FULHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top