• HABARI MPYA

  Saturday, April 10, 2021

  PULISIC APIGA MBILI CHELSEA YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 4-1


  CHELSEA imeibuka na ushindi wwa 4-1 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Kai Havertz dakika ya nane Christian Pulisic mawili dakika ya dakika ya 10 na 78 na Kurt Zouma dakika ya 30, wakati la Crystal Palace limefungwa na Christian Benteke dakika ya 63.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 31 na kurejea nafasi ya nne, ikizidiwa pointi mbili na Leicester City ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PULISIC APIGA MBILI CHELSEA YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top