• HABARI MPYA

  Thursday, April 01, 2021

  CAF YARUHUSU MASHABIKI 10,000 KUINGIA UWANJA WA MKAPA MECHI YA SIMBA SC NA AS VITA JUMAMOSI


  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeiruhusu timu ya Simba kuingiza mashabiki 10,000 katika mechi yao ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Hatua hiyo inafuatia maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya ZBC 2 inayopatikana kwenye kisimbuzi cha Azam Tv.
  Simba inayoongoza Kundi kwa pointi zake 10, tatu zaidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri inahitaji sare tu kujikatia tiketi ya Robo Fainali.
  AS Vita ni ya tatu ikiwa na pointi nne, mbele ya El Merreikh ya Sudan inayoshika mkia ikiwa na pointi moja tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YARUHUSU MASHABIKI 10,000 KUINGIA UWANJA WA MKAPA MECHI YA SIMBA SC NA AS VITA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top