• HABARI MPYA

  Saturday, April 24, 2021

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NEWCASTLE ANFIELD


  MABINGWA waliopoteza nafasi ya kutetea taji, Liverpool leo wamelazimishwa sare ya 1-1 na Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah alianza kuifungia Liverpool dakika ya tatu tu, kabla ya kiungo wa England, Joe Willock kuisawazishia Newcastle United dakika ya 90 na ushei.
  Liverpool inafikisha pointi 54 na kupanda nafasi ya sita, ikiizidi pointi moja Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi 33, wakati Newcastle United inafikisha pointi 36 katika mechi ya 33 pia, ingawa inabaki nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NEWCASTLE ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top