• HABARI MPYA

  Wednesday, April 14, 2021

  SIMBA SC WAREJEA NA MOTO LIGI KUU BARA, WAIKANDAMIZIA MTIBWA SUGAR MABAO 5-0 DAR


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamerejea na moto wao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara na leo wameichapa Mtibwa Sugar 5-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na nyota wa kigeni watupu, Wazambia Clatous Chama dakika ya tisa, Rally Bwalya dakika ya 19, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 43 na 52 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 69.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC inayofundishwa na Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 21 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA NA MOTO LIGI KUU BARA, WAIKANDAMIZIA MTIBWA SUGAR MABAO 5-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top