• HABARI MPYA

  Saturday, April 24, 2021

  MCHEZAJI WA BIASHARA UNITED YA MARA MSIMU ULIOPITA AFARIKI DUNIA AKIWA MAZOEZINI MUSOMA

  MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Biashara United Mara, Sospeter Maiga Mandala amefariki dunia asubuhi ya leo wakati akifanya mazoezi katika uwanja wa Posta mjini Musoma.
  Kwa mujibu wa wachezaji waliokuwa mazoezini na mchezaji huyo, Mandala alifika mazoezini kama kawaida akiendesha baiskeli yake na kufanya mazoezi  vizuri bila kuonyesha dalali  zozote lakini ghafla aliinama na kushika kifua.
   "Tumeanza mazoezi vizuri  asubuhi na leo alikuwa anakimbia sana na kutoa pasi,  lakini ghafla aliinama na kushika kifua, tulipokimbia kumuona akaonekana amepoteza fahamu, lakini tulipomfikisha hospitali ikaonekana amefariki dunia," alisema mchezaji huyo.
  x
  "Hata hivyo, hadi. sasa bado hatujapata taarifa za daktari aliyempokea ili kubaini nini kimesababisha kifo chake,".
  Mchezaji huyo inaelezwa hii ilikuwa Mara ya tatu kuanguka lakini wakati wote hakuwa wazi ili kupata matibabu ya tatizo la moyo linalosemekana lilikuwa linamsumbua, “ alisema mmoja wa wachezaji aliokuwa nao mazoezini kabla ya kifo chake.
  Mbali na Biashara, marehemu Mandala pia amewahi kuchezea timu za Nyakato FC, Kigera FC, JK FC, Pamba FC za Mwanza, Geita FC ya Geita, Stand United ya Shinyanga na Njombe Mji FC ya Njombe.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA BIASHARA UNITED YA MARA MSIMU ULIOPITA AFARIKI DUNIA AKIWA MAZOEZINI MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top