• HABARI MPYA

  Saturday, April 24, 2021

  MBEYA CITY WAITWANGA NAMUNGO FC 1-0 KATIKA LIGI KUU PALE PALE UWANJA WA MAJALIWA, RUANGWA

   

  BAO pekee la Juma Luizio dakika ya 12 limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 27 na kurejea nafasi ya 16 katika ligi ya timu 18, ambayo mwisho wa msimu timu nne zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu.
  Namungo yenyewe inabaki na pointi zake 31 za mechi 22 sasa katika nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAITWANGA NAMUNGO FC 1-0 KATIKA LIGI KUU PALE PALE UWANJA WA MAJALIWA, RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top