• HABARI MPYA

  Thursday, April 29, 2021

  BARCELONA YACHAPWA 2-1 NA GRANADA PALE PALE CAMP NOU

   WENYEJI, Barcelona wamechapwa 2-1 na Granada katika mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camp Nou.
  Mabao ya Granada yamefungwa na Darwin Machís dakika ya 63 na Jorge Molina dakika ya 79, wakati la Barcelona limefungwa na Nahodha wake, Lionel Messi dakika ya 23.
  Baada ya kipigo hicho Barcelona inabaki na pointi zake 71 katika nafasi ya tatu, nyuma ya Real Madrid yenye pointi 71 pia baada ya wote kucheza mechi 33, wakati Granada inafikisha pointi 45 za mechi 33 pia katika nafasi ya nane.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YACHAPWA 2-1 NA GRANADA PALE PALE CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top