• HABARI MPYA

  Friday, April 09, 2021

  JKT TANZANIA YAICHAPA MWADUI FC 3-1, BIASHARA UNITED YALAZIMISHA SARE KWA POLISI 1-1 MUSOMA


  TIMU ya JKT Tanzania imeichapa Mwadui FC mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya JKT yamefungwa na Daniel Lyanga mawili dakika ya 11 na 13 na Edson Katanga dakika ya 63, wakati bao pekee la Mwadui FC limefungwa na Feisal Rajab dakika ya 64 kwa penalti.
  Matokeo hayo yanaifanya JKT ifikishe pointi 27 baada ya kucheza mechi 25 na kupanda nafasi ya 12, wakati Mwadui inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi zake 16 za mechi 25 sasa.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Biashara United imelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Gerald Mathias alianza kuifungia Polisi dakika ya 66, kabla ya Tariq Simba kuisawazishia Biashara dakika ya 75.
  Biashara inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 24 ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Polisi inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 24 na inasalia nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA MWADUI FC 3-1, BIASHARA UNITED YALAZIMISHA SARE KWA POLISI 1-1 MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top