• HABARI MPYA

  Sunday, April 25, 2021

  TANZANIA PRISONS YAIBUKA NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA RUVU SHOOTING LEO SUMBAWANGA


  BAO pekee la Jeremiah Juma Mgunda dakika ya 51 limeipa ushindi wa 1-0 Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons imefikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 37 za mechi 27 pia katika nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAIBUKA NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA RUVU SHOOTING LEO SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top