• HABARI MPYA

  Wednesday, April 28, 2021

  MBEYA CITY YAFANYA BALAA ZITO LIGI KUU YA BARA, YAWATANDIKA JKT TANZANIA MABAO 6-1 UWANJA WA SOKOINE

   TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa 6-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 19, David Mwasa dakika ya 45 na ushei, Richardson Ng'ondya dakika ya 49, Juma Luizio dakika ya 68 na 88 na Pastory Athanas dakika ya 90 na ushei baada ya Danny Lyanga kuifungia JKT dakika ya nane.
  Kwa ushindi huo mnono, Mbeya City inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28 na kusogea nafasi ya 13, wakati JKT inabaki na pointi zake 27 za mechi 27 sasa katika nafasi ya 17.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAFANYA BALAA ZITO LIGI KUU YA BARA, YAWATANDIKA JKT TANZANIA MABAO 6-1 UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top