• HABARI MPYA

  Tuesday, April 13, 2021

  COASTAL UNION YAZINDUKA LIGI KUU NA KUWACHAPA WENYEJI, BIASHARA UNITED 1-0 LEO MUSOMA


  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imezinduka baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Issa Abushehe dakika ya 75 na kwa ushindi huo Coastal Union inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 25 na kupanda nafasi ya 11, wakati Biashara United inayobaki na pointi zake 40 za mechi 25 pia inaendelea kushika nafasi ya nne. 
  Ushindi huo unafuatia kichapo cha mabao 4-0 walichopewa na Gwambina katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAZINDUKA LIGI KUU NA KUWACHAPA WENYEJI, BIASHARA UNITED 1-0 LEO MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top