• HABARI MPYA

  Tuesday, April 27, 2021

  MWADUI FC YAKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA, YAICHAPA GWAMBINA 2-1 PALE PALE MISUNGWI

  TIMU ya Mwadui FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.
  Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Rashid Roshwa dakika ya 83 na Mohamed Hashim dakika ya 87 baada ya Gwambina kutangulia kwa bao la Meshack Abraham dakika ya 57.
  Mwadui FC inafikisha pointi 19 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 28, ingawa inaendelea kuzibeba timu nyingine zote 17 katika ligi hiyo ikihitaji miujiza tu kusalia msimu ujao.
  Gwambina yenyewe inabaki na pointi zake 30 za mechi 27 sasa katika nafasi ya 12.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI FC YAKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA, YAICHAPA GWAMBINA 2-1 PALE PALE MISUNGWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top