• HABARI MPYA

  Saturday, April 17, 2021

  CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 1-0 NA KUTINGA FAINALI FA ENGLAND

   

  TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Bao pekee la The Blues leo limefungwa na kiungo Mmorocco mzaliwa wa Uholanzi,  Hakim Ziyech dakika ya 55 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mjerumani, Timo Werner na sasa itakutana na mshindi kati ya Leicester City na Southampton zinazomenyana kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 1-0 NA KUTINGA FAINALI FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top