• HABARI MPYA

  Saturday, April 24, 2021

  SIMBA SC WAPANDA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA KUICHAPA GWAMBINA FC 1-0 MISUNGWI

   

  MABINGWA watetezi, Simba SC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki wa kushoto na Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein 'Tshabalala' aliyefunga dakika ya 29 kwa shuti la umbali wa mita 35 baada ya pasi ya kiungo Muzamil Yassin.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 24, ikiwazidi pointi moja vigogo, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.
  Tshabalala anafunga bao hilo siku mbili tu baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumia klabu hiyo hadi mwaka 2024.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPANDA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA KUICHAPA GWAMBINA FC 1-0 MISUNGWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top