• HABARI MPYA

  Tuesday, April 27, 2021

  SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-1 NA KUPOTELEA ANGANI

   

  MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuitandika Dodoma Jiji FC 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya nane na 67 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 66, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Cleophace Mkandala dakika ya 29.
  Simba SC inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 25 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya watani wao jadi, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
  Dodoma Jiji yenyewe inabaki na pointi zake 38 za mechi 28 sasa katika nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA DODOMA JIJI 3-1 NA KUPOTELEA ANGANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top