• HABARI MPYA

  Saturday, April 17, 2021

  COASTAL UNION YAWACHAPA RUVU SHOOTING 2-1 LIGI KUU LRO UWANJA WA MKWAKWANI  WENYEJI, Coastal Union wamewachapa Ruvu Shooting 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijiji Tanga.
  Mabao ya Coastal Union leo yamefungwa na Rashid Chambo dakika ya 42 na Ayoub Masoud dakika ya 63, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Fully Zullu Maganga dakika ya 21.
  Kwa ushindi huo Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda inafikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 26 na kusogea nafasi ya tisa kutoka ya 11, wakati Ruvu Shooting ya kocha Charles Boniface Mkwasa inabaki na pointi zake 34 za mechi 25 sasa katika nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAWACHAPA RUVU SHOOTING 2-1 LIGI KUU LRO UWANJA WA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top