• HABARI MPYA

  Sunday, April 04, 2021

  NAMUNGO FC MAMBO MAGUMU AFRIKA, YAPIGWA TENA NA LEO NYUMBANI 1-0 NA NKANA FC YA ZAMBIA


  TIMU ya Namungo FC imepoteza mechi ya tatu mfululizo katika Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Nkana FC ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Bao pekee la Nkana FC leo limefungwa na mshambuliaji Diamond Chikwekwe dakika ya 69 na matokeo hayo yanaifanya timu ya Ruangwa mkaoni Lindi iendelee kushika mkia kufuatia kufungwa 1-0 na Raja Athletic Jijini Casablanca nchini Morocco na 2-0 na Pyramids ya Misri hapa hapa Dar es Salaam katika mechi zake mbili za awali.
  Nkana sasa ni ya tatu baada ya kukusanya pointi tatu za kwanza leo kufuatia nayo kufungwa 3-0 na Pyramids nchini Misri na 2-0 na Raja kwao, Zambia katika mechi zake mbili za awali.
  Raja na Pyramids zenye pointi sita kila zinamenyana muda huu Jijini Casablanca katika mchezo utakaozitenganisha timu hizo za Kaskazini mwa Afrika nafasi ya kwanza na ya pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC MAMBO MAGUMU AFRIKA, YAPIGWA TENA NA LEO NYUMBANI 1-0 NA NKANA FC YA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top