• HABARI MPYA

  Wednesday, April 14, 2021

  IDDI NADO ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI KUENDELEA KUPIGA KAZI KWENYE KIKOSI CHA AZAM FC


  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Idd Suleiman 'Nado' amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Azam FC.
  Nado alisaini mkataba huo jana mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.
  Nado aliyejiunga na Azam FC msimu uliopita akitokea Mbeya City, amekuwa mchezaji muhimu kikosini na hadi sasa msimu huu akiwa amehusika kwenye mabao 12 ya timuhiyo, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IDDI NADO ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI KUENDELEA KUPIGA KAZI KWENYE KIKOSI CHA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top