• HABARI MPYA

  Friday, April 16, 2021

  MAN UNITED YATINGA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Manchester United imekwenda Nusu Fainali ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Granada ya Hispania usiku huu Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Edinson Cavani dakika ya sita na Jesús Vallejo aliyejifunga dakika ya 90 na kwa matokeo hayo, Mashetani Wekundu wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda pia 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Hispania wiki iliyopita.
  Sasa Manchester United itakutana na AS Roma ya Italia iliyoitoa Ajax ya Uholanzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATINGA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top