• HABARI MPYA

  Sunday, April 11, 2021

  NAMUNGO FC YAENDELEA KUGAWA POINTI KUNDI D KOMBE LA SHIRIKISHO, NA LEO IMECHAPWA 1-0 NA NKANA FC NDOLA


  TIMU ya Namungo FC imeendelea kugawa pointi katika mechi za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya leo pia kuchapwa 1-0 na wenyeji, Nkana FC Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola, Zambia.
  Bao pekee la Nkana FC leo limefungwa na kiungo Freddy Tshimenga dakika ya 71 akimalizia pasi yaHarrison Musonda Chisala.
  Nkana FC imefikisha pointi sita, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Aprili 4 dhidi ya timu hiyo ya Tanzania ikitoka kuchapwa 3-0 na Pyramids nchini Misri na 2-0 na Raja Athletic hapo hapo Ndola.
  Namungo FC inaendelea kushika mkia baada ya kupoteza mechi zote nne za awali, ikiwemo kuchapwa 1-0 na Raja Athletic nchini Morocco na 2-0 na Pyramids Dar ed Salaam.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, wenyeji, Pyramids wamechapwa 3-0 na Raja Atheltic Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo.
  Raja inaendelea inaongoza kundi kwa sasa baada ya kukusanya pointi 12 kufuatia kuzifunga zote, Namungo, Pyramids mara mbili na Nkana FC mara moja. 
  Pyramids na Nkana FC kila moja ina pointi sita katika nafasi ya pili na ya tatu na Namungo ambayo haina pointi inashika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAENDELEA KUGAWA POINTI KUNDI D KOMBE LA SHIRIKISHO, NA LEO IMECHAPWA 1-0 NA NKANA FC NDOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top