• HABARI MPYA

  Monday, April 26, 2021

  GRIEZMANN APIGA MBILI BARCA YASHINDA 2-1 LA LIGA


  MABAO ya Mfaransa Antoine Griezmann dakika za 28 na 35 jana yaliipa Barcelona ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal ambayo bao lake lilifungwa na Mnigeria Samuel Chukwueze dakika ya 26 katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Ceramica Jijini Villarreal.
  Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 71 baada ya kucheza mechi 32, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Real Madrid, wakati Atletico Madrid inaendelea kuongoza kwa pointi zake 73 za mechi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRIEZMANN APIGA MBILI BARCA YASHINDA 2-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top