• HABARI MPYA

  Wednesday, April 28, 2021

  REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA CHELSEA NYUMBANI

  WENYEJI, Real Madrid wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid nchini Hispania.
  Kiungo Mmarekani Christian Pulisic alianza kuifungia Chelsea dakika ya 14, kabla ya mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema kuisawazishia Real Madrid dakika ya 29 sasa timu hizo zitarudiana Mei 5 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, The Blues wakihitaji hata sare ya 0-0 kwenda Fainali.
  Nusu Fainali nyingine ya kwanza inachezwa leo Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa baina ya wenyeji, Paris Saint-Germaine na Manchester City Saa 4:00 usiku.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA CHELSEA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top