• HABARI MPYA

    Friday, October 04, 2019

    NDAYIRAGIJE AMUONGEZA KIKOSINI DITRAM NCHIMBI ALIYEWAPGA HAT TRICK YANGA JANA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mrundi wa timu ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amemuongeza mshambuliaji Ditram Nchimbi anayecheza Polisi Tanzania ya Kilimanjaro kwa mkopo kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
    Ndayiragije amefanya uamuzi huo siku moja tu baada ya Nchimbi kufunga mabao matatu katika sare ya ugenini ya 3-3 dhidi ya wenyeji, Yanga SC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
    Nchimbi anaungana na wachezaji wengine 28 ambao Ndayiragije aliwaita jana ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Rwanda mjini Kigali Oktoba 14 kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Sudan Oktoba 18 nchini Uganda.


    Ditram Nchimbi (kulia) ameitwa Taifa Stars baada ya kuifungia Polisi Tanzania 'hat trick' dhidi ya Yanga jana 

    Mechi ya kwanza Taifa Stars ilifungwa 1-0 nyumbani Dar es Salaam na natakiwa kwenda kushinda 2-0 ugenini ili kukata tiketi ya kucheza fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee. 
    Kikosi kamili cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Rwanda ambacho kitamenyana pia na Sudan kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga SC) na Said Kipao (Kagera Sugar).
    Mabeki; Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Shomari Kapombe (Simba SC), Gardiel Michael (Simba SC), Mohammed Hussein (Simba SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).
    Viungo; Himid Mao (ENPPI/Misri), Jonas Mkude (Simba SC), Farid Mussa (Tenerife/Hispania), Adi Yussuf (Solihull Moors/England), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Muzamil Yassin (Simba SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC), Feisal Salum (Yanga SC) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi/Morocco)  
    Washambuliaji; Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Kelvin John (Huru), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Andrew Simchimba (Azam FC), Miraj Athumani (Simba SC) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDAYIRAGIJE AMUONGEZA KIKOSINI DITRAM NCHIMBI ALIYEWAPGA HAT TRICK YANGA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top