• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 23, 2019

  NAMUNGO FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0, POLISI NA ALLIANCE NAZO ZANG’ARA NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, RUANGWA
  BAO pekee la mshambuliaji Bigirimana Blaise dakika ya 27 limeipa ushindi wa 1-0 Namungo FC dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kupanda kileleni ikiwazidi kwa pointi moja tu mabingwa watetezi, Simba SC ambao wapo uwanjani hivi sasa wanamenyana na Azam FC.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Baraka Majogoro dakika ya 76 limeipa ushindi wa 1-0 Polisi Tanzania 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

  Naye Israel Patrick akafunga bao la mapema tu dakika ya tatu, Alliance FC ikiilaza 1-0 Ruvu Shooting Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Na Bao la mkwaju wa penalti la dakika ya 74 la mkongwe, Kigi Makasi likainusuru Ndanda FC kulala mbele ya Lipuli FC iliyotangulia kwa bao la Paul Nonga dakika ya 42 timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Nangwnada Sijaona mjini Mtwara.
  Mechi nyingine mbili zikamalizika sare ya bila ambazo ni kati ya Tanzania Prisons na Biashara United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Coastal Union na Singida United Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0, POLISI NA ALLIANCE NAZO ZANG’ARA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top