• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 20, 2019

  BIASHARA YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 SOKOINE, COASTAL UNION NA POLISI ZASHINDA 2-1 NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Biashara United imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mbeya City 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. 
  Ushindi huo unaokuja baada ya timu hiyo kupoteza mechi nne na kutoa sare moja, umetokana na mabao ya Ally Kombo dakika ya 67 na Innocent Edwin dakika ya 89.
  Nao Coastal Union wameutumia vyema uwanja wa nyumbani, Mkwakwani mjini Tanga baada ya kuichaoa Mwadui FC 2-1.  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shaaban Idd dakika ya nane na beki Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 59, baada ya Mwadui FC kutangulia kwa bao la Gerald Mdamu dakika ya tatu.
  Nayo Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida United Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Mishi, mabao yake yakifungwa na Marcel Kaheza dakika ya 23 na Erick Msagati dakika ya 89, kufuatia Stephen Opuku kuanza kuwafungia wageni dakika ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BIASHARA YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 SOKOINE, COASTAL UNION NA POLISI ZASHINDA 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top