• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 21, 2019

  VIGOGO KIBAO VYATUPWA NJE FAINALI ZA CHAN MWAKANI CAMEROON

  MECHI za kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon zimekamilika mwishoni mwa wiki, huku mataifa yenye majina makubwa kama Nigeria, Senegal, Ivory Coast na Ghana yakikosa nafasi.
  Timu Zilizofuzu michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee zitakazoanza Januari 2020 pamoja na wenyeji, Cameroon ni Tanzania, Uganda, Uganda, Rwanda, Zambia, Namibia, Morocco, Zimbabwe, DRC, Kongo Tunisia, Burkina Faso, Guinea, Niger, Mali na Togo watakaoshiriki kwa mara ya kwanza.
  Ghana walishindwa kufuzu kwa mara ya tatu kuanzia mwaka 2016, wakitolewa na Burkina Faso, kufuatia sare ya 0-0 nyumbani mjini Ouagadougou wakitoka kushinda 1-0 ugenini mjini Kumasi.
  Senegal wametolewa kwa penalti na Guinea mjini Conakry baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
  Tembo wa Ivory Coast walishindwa kupindua kipigo cha 2-0 ugenini mbele ya Niger baada ya kuambulia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa marudiano nyumbani. 
  Mjini Sale nchini Morocco Anice Badri aliifungia Tunis amabao mawili ikiichapa Libya 2-1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani. 
  Mjini Bamako, Mali iliendeleza burudani safi ya mchezo ikiichapa Mauritania 2-0 kukata tiketi ya Cameroon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIGOGO KIBAO VYATUPWA NJE FAINALI ZA CHAN MWAKANI CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top