• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 26, 2019

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-0 MCHEZO WA LIGI KUU LEO MJINI MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Mtibwa Sugar leo imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.  
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha Zubery Katwila inafikisha pointi nane katika mchezo wa nane na kujivuta hadi nafasi ya 12, ikiishusha Yanga yenye pointi saba za mechi nne. 
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Mtibwa Sugar mabingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo 1999 na 2000 yamefungwa na Jaffary Salum Kibaya dakika ya 55 akimalizia  pasi ya kiungo Abdulhalim Humud ‘Gaucho’, aliyefunga la pili dakika ya 89 kwa pasi ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
  Abdulhalim Humud leo ameseti bao moja na kufunga moja Mtibwa Sugar ikishinda 2-0 dhidi ya Polisi

  Pamoja na kocha Suleiman Matola kuwaanzisha washambuliaji wake hatari, Ditram Nchimbi na Marcel Kaheza, lakini hawakuweza kuinusuru na kipigo cha ugenini leo, ambacho kinakuwa cha pili msimu huu.
  Maana yake, Polisi Tanzania yenye maskani yake Moshi mkoani Kilimanjaro iliyopanda Ligi Kuu msimu huu inabaki na pointi zake 10 baada ya kiucheza mechi sita.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa;  Shaaban Kado, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Daudi, Cassian Ponera, Abdulhalim Humud, Salum Kihimbwa/Salum Kanoni dk90+5, Ally Yussuf, Juma Luizio/Ismail Mhesa dk70, Jaffar Kibaya/Riphat Msuya dk56 na Awadh Juma.
  Polisi Tanzania; Ally Yussuf, William Lucian ‘Gallas’, Yassin Salum, Pato Ngonyani, Mohammed Kassim, Baraka Majogoro, Andrew Chamungu/Erick Msagati dk75, Hassan Maulid, Ditram Nchimbi, Marcel Kaheza/Mohammed Mkopi dk60 na Sixtus Sabilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-0 MCHEZO WA LIGI KUU LEO MJINI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top