• HABARI MPYA

    Saturday, October 12, 2019

    SIMBA SC YAENDELEA KUWAPA RAHA MASHABIKI WAKE, YAICHAPA BANDARI YA KENYA 1-0 TAIFA

    Na Asha Kigundula, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Simba SC kimeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bandari ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Ibrahim Ajibu Migomba dakika ya 76 akimalizia pasi ya kiungo Rashid Juma. 
    Simba SC ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama wachezaji wake wangetumia vyema nafasi zote walizopyta, hususan viungo Deo Kanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkenya Francis Kahata.

    Kahata alipoteza nafasi nzuri za kufunga dakika ya 15 aliposhindwa kumalizia pasi ya Deo Kanda,  dakika ya 20 alipopiga juu, dakika ya 21 shuti lake lilipopanguliwa na kipa Michael Wantika na dakika ya 40 shuti lake lilipookolewa tea na mlinda mlango wa Bandari. 
    Kwa upande wake Kanda aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, ambaye kama Kahata aliyetokea Gor Mahia ya kwao wote wapo katika msimu wao wa kwanza Msimbazi, alipoteza nafasi ya kufunga kuanzia dakika ya tano baada ya kupiga juu na dakika ya 38 alipopiga shuti hafifu mpira ukatoka nje.
    Naye kiungo mwingine aliye katika msimu wake wa kwanza Msimbazi, Sharaf Eldion Shiboub naye poia hakuwa na siku nzuri – lakini kwa ujumla Simba SC iliyokosa nyota wake wengi wa kikosi cha kwanz aambao wapo na timu zao za taifa ilicheza vizuri.
    Baada ya mchezo huo, kikosi cha Simba SC chini ya kocha wake Mbelgiji, Patrick Aussems kitaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa ajili ya michezo miwili zaidi ya kirafiki, dhidi ya Mashujaa FC Jumatatu na Aigle Noir FC ya Burundi Jumatano Uwanja wa Lake Tanganyika.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Haruna Shamte, Joseph Peter/Yusuph Mlipili dk46, Tairone Santos, Paschal Wawa, Gerson Fraga ‘Viera’, Deo Kanda, Sharif Shiboub, Wilker Da Silva/Said Ndemla dk57, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata.
    Bandari FC; Michael Wantika, Atariza Amai, Fred Wilata, Brian Otieno, Felly Mlumba, Collins Agade, Patrick Mugendi/Cliff Kasuti dk46, Willy Lugogo, Wycliffe Ochomo, William Wadri na Darius Msagita/Simban Kenga dk46.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEA KUWAPA RAHA MASHABIKI WAKE, YAICHAPA BANDARI YA KENYA 1-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top