• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 31, 2019

  RODRYGO AFUNGA REAL MADRID YAICHAPA LEGANES 5-0 LA LIGA

  Kinda Mbrazil, Rodrygo Silva de Goes aliyeoandishwa kutoka timu B akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya saba katika ushindi 5-0 dhidi ya Leganes kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu. Mabao mengine ya Real yalifungwa na T. Kroos dakika ya nane, Nahodha Sergio Ramos kwa penalti dakika ya 24, mkongwe Karim Benzema kwa penalti pia dakika ya 69 na Luka Jovic dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo kikosi cha kocha Zinadine Zidane kinafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10, sasa kikizidiwa pointi moja na vinara, Barcelona amabo pia ni mabingwa watetezi 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RODRYGO AFUNGA REAL MADRID YAICHAPA LEGANES 5-0 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top