• HABARI MPYA

  Sunday, October 27, 2019

  YANGA SC YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFRIKA, YACHAPWA 2-1 NA PYRAMIDS FC MWANZA

  Na Asha Said, MWANZA
  YANGA SC imejiweka kwenye mazingira magumu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi hiyo jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Yanga sasa wanaendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi za nyumbani za michuano ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa ambako ushindi wa ugenini wa 1-0 uliwavusha Raundi ya pili baada ye sare ya 1-1 nyumbani na Township Rollers kabla ya kwenda kutolewa na Zesco United kufuatia kufungwa 2-1 Ndola ikitoka kutoka sare ya 1-1 Dar es Salaam.
  Na pamoja na kuuhamishia Mwanza mchezo wake wa kwanza mchujo wa kuwania hatua ya makundi, Yanga SC leo imeshindwa kugeuza matokeo, zaidi yamekuwa mabaya kabisa baada ya kufungwa kutoka sare za Dar es Salaam. 


  Sasa Yanga SC watatakiwa kwenda kujaribu kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano Novemba 3, mwaka huu Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo kwa mechi zao za nyumbani.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Pyramids FC yalifungwa na kiungo Mburkinabe, Eric Traore dakika ya 42 na beki Omar Gaber dakika ya 63  wote walimalizia krosi za mshambuliaji Mohamed Farouk, wakati bao pekee la Yanga lilifungwa na kiungo wake, Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Yanga SC inayofundishwa na kocha Mkongo, Mwinyi Zahera, ilimaliza pungufu baada ya beki wake mzoefu, Kelvin Yondan kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90 na ushei.
  Kikosi cha Yanga SC; Farouk Shikalo, Juma Abdul, Ally Mtoni ‘Sonso’, Kelvin Yondani, Ally Ally, Feisal Salum/Juma Balinya dk68, Mrisho Ngassa/Deus Kaseke dk71, Abdulaziz Makame/Patrick Sibomana dk87, Sadney Urikhob, Papy Tshishimbi na Mapinduzi Balama.            
  Pyramids FC; Ahmad El Shenawy, Omar Gaber, Abdullah Bakri, Donga Nabeel, Eric Traore, Mohammed Fathi, Abdallah Saed/Ahmed Tawfik dk80, Mohamed Farouk/Mohamed Hamdy dk90+3, Mohammed El Gabbas/Antwi Johe dk69, Rajab Bakar na Ahmed Mansour.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFRIKA, YACHAPWA 2-1 NA PYRAMIDS FC MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top