• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 19, 2019

  MINZIRO NDIYE KOCHA MPYA WA PAMBA SC ‘TP LINDANDA ’BAADA YA MUHIBU KANU KUONDOKA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  UONGOZI wa Pamba SC ‘TP Lindanda’ ya Mwanza umeingia mkataba na Fred Felix Minziro kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Muhibu Kanu aliyeondoka.
  Taarifa ya Pamba SC imesema kwamba Kamati ya Utendaji ya klabu imeridhishwala na rekodi za makocha hao wazawa na kuamua kuingia nao mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika mwisho wa msimu huu wa 2019/2020.
  Fred Felix Minziro, mchezaji wa zamani wa Yanga SC aliyewahi kuifundisha klabu hiyo pamoja na Tanzania Prisons, JKT Ruvu kabla ya kwenda kuzipandisha Ligi Kuu, Singida United na KMC atasaidiwa na Ally Kisaka.

  Kaimu Mwenyekiti wa Pamba SC Aleem Alibhai ‘Try Again’ (katikati) akiwa na Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo, Fred Felix Minziro (kushoto) na Msaidizi wake Ally Kisaka (kulia) 

  “Ally Kisaka huyu unaweza ukasema Mwenye Mji wake Amerudi Baada ya Kuwapa Furaha Wana Mwanza kwa kufanikisha timu ya Pamba kufika katika hatua ya Mtoano (Playoff) na kuifanya Pamba SC Kuweka Rekodi ya kutofungwa katika Uwanja wa Nyamagana Sasa atakua Kocha msaidizi wa timu,”imesema taarifa hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MINZIRO NDIYE KOCHA MPYA WA PAMBA SC ‘TP LINDANDA ’BAADA YA MUHIBU KANU KUONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top