• HABARI MPYA

  Sunday, October 27, 2019

  YANGA SC UAMUZI NI WENU KUSUKA AMA KUNYOA DHIDI YA PYRAMIDS FC

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE wakati umewadia,wanasema muda haudanganyi ni kweli umewadia,ile mechi inayokwenda kuamua hatima ya Yanga SC kutinga makundi au laaa imewadia ni leo ndani ya Kirumba kwani ni dakika 180 huku 90 zikiwa za Kirumba na 90 zikiwa kule nchini Misri ndizo zitakazoamua nani atinge hatua ya makundi.
  Mara zote nimekuwa nikieleza kuwa ni rahisi kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa ambayo sehemu kubwa ya mechi zake ni mtoano kuliko hata kushinda taji la ligi kuu,kwani mipango ya mechi hizi huwa zaidi ni mechi baada ya mechi ukifanikiwa kujua ubora na udhaifu wa timu pinzani na kuandaa mbinu bora dhidi yao tayari unakuwa kwenye nafasi ya kufanya vema katika mchezo husika huku ukitumia wachezaji sahihi katika kikosi chako ili kusaka matokeo ya ushindi.

  Katika mchezo wa leo ni dhahiri Pyramid FC wataingia na taadhari na kujivunia uwezo wao wa kuficha mpira ili kuhakikisha Yanga SC wanakosa kasi ya kushambulia huku wakiwaruhusu Yanga SC wacheze kwenye eneo lao bila kuleta madhara kwenye eneo la 18 la timu yao,hii ndiyo imekuwa silaha kubwa sana ya Pyramid FC huku wakitumia zaidi mipira ya adhabu ndogo na kona ili kupata matokeo.
  Kwa tafsiri hiyo Yanga SC wanatakiwa kuja tofauti kwa kupunguza umiliki wa mpira usio na faida katika eneo lao na kujaribu kucheza direct football huku wakitumia winga zote mbili kupitishia mashambulizi na kuwachosha wapinzani wao ili kuwasababishia wafanye makosa sehemu yao ya ulinzi na kupata matokeo .
  Katika eneo la katikati ya uwanja likionekana dhahiri kuwa litakuwa na ushindani mkubwa sana kutokana timu ya Pyramid FC kutamani kulimiliki eneo hilo ili kuwamaliza Yanga SC kwani mara nyingi mashambulizi mengi huanzia katikati ya kiwanja na hapa ndipo Kocha wa Yanga SC Mwinyi Zahera anatakiwa kuwa makini na uchaguzi wa wachezaji wawili hadi watatu katika eneo hili ambao watalazimika kutengeneza mwenendo wa timu na kutengeneza uwiano wa kujilinda na kushambulia kwa kasi kwani ni dhahiri Pyramids FC watakuwa wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza hivyo mwalimu anatakiwa kuchagua viungo ambao watapora mipira na kuwa wepesi kuisambaza kama ningepewa nafasi ya kuchagua nani aanze basi namuona Makame,Banka wakilikamata eneo hili la chini kwani kiwango cha Feisal katika siku za karibuni kimekuwa duni na muda mwingi amekuwa akisababisha timu kushambuliwa kutokea kwake na Tshishimbi pia. 
  Ukiwaangalia Pyramids FC katika eneo la kati ndipo msingi wa timu yao ulipo,hasa wanapokuwa ugenini na ndio maana hata kikosi chao chote kina viungo 11 na washambuliaji 3 Chini ya uongozi wa kiungo wao punda Nabil Donga akishirikiana na Ibrahim Hassan,Mohammed Fathy pamoja na Islam Eisa kuhakikisha wanaichukua mechi kwa muda wote wa mchezo jambo ambalo ambalo linawalazimu Yanga sc kuhakikisha mipira aitulii katika eneo hilo na kuwalazimisha viungo wa Pyramids wanakosa utulivu na uwezo wa kuchezea mpira uku wakiwagonga mda wote na kuwatoa mchezoni jambo ambalo litawafanya wawe na option moja tu ya kujilinda kuliko kushambulia na kutoa nafuu kwa wachezaji wa Yanga SC kuwa na option nyingi za kushambulia.
  Kwenye eneo la umaliziaji la Yanga kumekuwa na matatizo kadhaa kwenye mechi yao na Mbao FC ambayo mwalimu alikiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuahidi kuyatatua haraka,lakini bila shaka wanapaswa kuongeza umakini uku wakutanua wigo wa kushambulia na kutoa fursa kwa yeyote anayepata nafasi kuweza kuzitumia kwani hadi sasa hakujapatikana combination ya wachezaji wa eneo hilo kuwa na mbinu za kuipatia Timu matokeo hivyo kikubwa ni kushambulia kwa kasi na kutumia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kuweza kufunga Sadney,Balinya,Ngasa,Sibomana wote ni wafungaji wazuri ambao kama wakiongeza umakini wanaweza kuipa matokeo Yanga SC katika mchezo wa leo.
  Huku Pyramids wakiwa na ubora mkubwa katika eneo hili ambao limekuwa likitegemea zaidi mipango thabiti ya eneo la kati ya kiwanja huku watu wao hatari wa kuweka mipira kambani ni John Antwi na Dodo Elgabas hawa jamaa hawana masihara kabisa ingawa bado hawana kasi sana na kuweza kudhibitiwa kwa kufanyiwa man to man marking uku Yondani akiwa kiongozi wa zoezi hili uku wakiwachezea tafu mda wote na kuwatengenezea uwoga na bado uwanja utatoa faida kwa Yanga SC tofauti na Pyramids ambao wataamua kutumia mipira ya juu ili kupunguza makosa na kupoteza mipira.
  Yote kwa yote Yanga SC wanapaswa kuwa makini katika jukumu hili la kitaifa uku wakicheza kitimu zaidi na kupunguza makosa katika sehemu ya ulinzi uku silaha kubwa ikiwa ni kutumia nafasi zitakazo patikana kwani kuruhusu bao lolote la ugenini kwa Pyramids ni madhara makubwa sana katika mechi ya marudiano kule nchini Misri.
  Naamini bado Yanga SC wanaweza kufanya kitu na kutoa furaha kwa Watanzania katika mechi ya leo. MUNGU ibariki Tanzania MUNGU ibariki Yanga SC
  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia Akaunti yake ya instagram kama @dominicksalamba na simu namba +255713942770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC UAMUZI NI WENU KUSUKA AMA KUNYOA DHIDI YA PYRAMIDS FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top