• HABARI MPYA

  Wednesday, October 16, 2019

  WAMBURA AONDOLEWA BODI YA LIGI NA KUREJESHWA IDARA YA HABARI TFF, MILAMBO AULA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AFISA Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura amemaliza mkataba wake wa kuitumikia nafasi hiyo na sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF akisaidiwa na Cliford Ndimbo atakayehusika na habari pamoja na Aron Nyanda atakayeshughulika na masoko.
  Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema nafasi ya CEO wa Bodi ya Ligi iliyokuwa ikishikiliwa na Wambura itatangazwa baadaye.
  Kidao pia amesema Kamati ya Utendaji ya TFF imemthibitisha Oscar Mirambo kuwa Mkurugenzi wa ufundi. Awali Mirambo alikuwa akiikaimu nafasi hiyo.

  Aidha, Kidao ameweka wazi mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusu mfumo wa uongozi kuelekea uchaguzi ujao.
  Moja kati ya mambo yaliyoguswa ni nafasi ya Makamu wa Rais ambapo kuanzia sasa hatachaguliwa kwa kupigiwa kura bali atakuwa akiteuliwa na Rais.
  Mabadiliko mengine yamegusa idadi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ambayo sasa itapungua kutoka 22 hadi 13, huku kanda nazo zikipunguzwa kutoka 13 hadi 6.
  Vilevile katika mabadiliko hayo wajumbe wa mkutano mkuu watapungua kutoka 129 hadi 87, ikimaanisha kuwa kila mkoa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara utatoa wajumbe wawili, wajumbe 20 watatoka kwenye vilabu huku vyama washirika wakitoa wajumbe 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAMBURA AONDOLEWA BODI YA LIGI NA KUREJESHWA IDARA YA HABARI TFF, MILAMBO AULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top