• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 31, 2019

  LIVERPOOL YAING'OA ARSENAL KWA MATUTA CARABAO BAADA YA SARE YA 5-5

  Curtis Jones akipongezwa na wenzake baada ya kufunga penalti ya ushindi Liverpool ikiichapa Arsenal kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 5-5 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao usiku wa jana Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool yalifungwa na Shkodran Mustafi aliyejifunga dakika ya sita, James Milner kwa penalti dakika ya 43, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 58 na Divock Origi dakika ya 62 na 90 na ushei, wakati ya Arsenal yalifungwa na Lucas Torreira dakika ya 19, Gabriel Martinelli dakika ya 26 na 36, Ainsley Maitland-Niles dakika ya 54 na Joe Willock dakika ya 70.
  Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Adam Lallana, Rhian Brewster, Origi na Curtis Jones, wakati za Arsenal zilifungwa na Héctor Bellerin, Mattéo Guendouzi, Martinelli na Maitland-Niles huku , Dani Ceballos pekeea akikosa 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAING'OA ARSENAL KWA MATUTA CARABAO BAADA YA SARE YA 5-5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top