• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 31, 2019

  SAMATTA AFUNGA BAO MUHIMU KRC GENK YATOKA NYUMA NA KUPATA SARE YA 2-2 NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao la kwanza la kusawazisha, timu yake, KRC Genk ikitoka nyuma kwa 2-0 na kipata sare ya 2-2 na wageni, Royal Antwerp FC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alifunga bao hilo dakika ya 69 akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen kabla ya kiungo Mnorway, Sander Berge kuisawazishia Genk dakika ya 90 na ushei.
  Na hiyo ilifuatia Royal Antwerp FC kutangulia kwa mabao ya mshambuliaji Mcameroon, Didier Lamkel Ze dakika ya nane akimalizia pasi ya beki Muangola, Aurelio Buta na mshambuliaji Mreno, Ivo Rodrigues dakika ya 47 akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Alexis De Sart.

  Kwa sare hiyo, Genk inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 12 wakiwa wanazidiwa pointi moja na Antwerp inayolingana na Sporting Charleroi na AA Gent.
  Club Brugge inaendelea kuongoza Ligi Daraja la A Ubelgiji kwa pointi zake 30 za mechi 12, ikifuatiwa na Standard Liege yenye pointi 27 za meci 13 na Mechelen yenye pointi 23 za mechi 13.
  Samatta jana amecheza mechi ya ya 171 jumla kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 69.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 134 na kufunga mabao 53, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Europa League mechi 24 na mabao 14 na Ligi ya Mabingwa Ulaya tatu tu akiwa amefunga bao moja.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Coucke, De Norre, Dewaest, Lucumi, Uronen/Wouters dk45, Berge, Heynen, Ito/Bongonda dk58, Ndongala/Odey dk83, Samatta na Onuachu.
  Royal Antwerp FC; Bolat, De Laet, Lamkel Zé/Hongla dk96, Rodrigues, Arslanagic, Hoedt, De Sart, Aurelio, Haroun, Mbokani na Mirallas.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO MUHIMU KRC GENK YATOKA NYUMA NA KUPATA SARE YA 2-2 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top