• HABARI MPYA

    Saturday, October 12, 2019

    SIMBA NA YANGA ZAONGOZA KUTOA WACHEZAJI WENGI TIMU YA TAIFA CHALLENGE YA WANAWAKE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Bakari Nyundo Shime ameita kikosi cha awali cha wachezaji 39 kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake (CECAFA Challenge Womens) 2019 inayotarajiwa kuanza Novemba 16 hadi 28 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
    Shime anayesaidiwa na Edna Lema katika kikosi hicho cha Kilimanjaro Queens amechukua wachezaji 10 kutoka Simba Queens ambao ni Janeth Shijja, Vaileth Thadeo, Harrieth Shijja, Zubeda Mgunda, Fatuma Issa ‘Densa’, Julie Singano, Mwanahamisi Omary, Opa Clement, Thabea Hamdani na Dotto Tossy.
    Wachezani wengine saba wametoka kwa mahasimu wa Simba Queens, Yanga Princess ambao ni Amina Ally, Tausi Abdallah, Happiness Hezron, Anastazia Nyandago, Irene Kisisa, Lucia Mrema na Neema Charles.

    JKT Queens imetoa wachezanji watano ambao ni Najat Abbas, Deonisia Minja, Anastazia Katunzi, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Stumai Abdallah sawa na Mlandizi Queens ambayo kwao wamechukuliwa Janeth Christopher, Philomena Daniel, Emiliana Mdimu, Masha Omary na Asha Ismail.
    Wachezaji wengine watano Shamim Ally, Eva Jackson, Diana Lucas, Protasia Mbunda na Famukazi Ally wametoka Ruvuma, wakati wane wametoka Alliance ambao ni Enekia Kasonga, Esther Mabanza, Aisha Mashaka na Rahabu Joshua.
    Wengine ni Judith Nyato kutoka Panama ya Tandika, Asha Hamza kutoka Kigoma Sisters na Joyce Meshack wa sekondari ya Makongo mjini Dar es Salaam.
    Challenge ya wanawake itafanyika kwa mara ya tatu tu kihistoria mwaka huu baada ya 2016 Jinja nchini Uganda na 2018 mjini Kigali, Rwanda mar azote Kilimanjaro Queens wakibeba taji hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZAONGOZA KUTOA WACHEZAJI WENGI TIMU YA TAIFA CHALLENGE YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top