• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 17, 2019

  BONDIA AFARIKI DUNIA SIKU NNE TU BAADA YA KIPIGO KIKALI ULINGONI

  BONDIA Mmarekani, Patrick Day amefariki dunia jana Jumatano zikiwa zimepita siku nne tangu atolewe na machela ulingoni baada ya kupigwa na mpinzani wake Charles Conwell katika raundi ya 10 ya pambano lao. 
  Katika pambano hilo la uzito Super Welter na la utangulizi kabla ya Oleksandr Usyk kuzipiga na Chazz Witherspoon lililofanyika mjini Wintrust Arena, Chicago, Marekani, Patrick mwenye umri wa miaka 27 alipoteza fahamu baada ya kupata majeraha ya ubongo na hivyo kukimbizwa Hospitali ambako alilazwa hadi umauti ulipomfika.

  Taarifa iliyotolewa na Promota wake Lou DiBella inasema kuwa, Patrick alifariki akiwa amezungukwa na familia yake, marafiki zake wa karibu na watu wa timu yake ya ngumi.
  Wakati Patrick alipokuwa mahututi hospitali, mpinzani wake Mmarekani Charles Conwell,21, aliandika barua ya masikitiko, akisema hakutaka kitu hicho kimtokee Patrick na kueleza kuwa tukio hilo limemfanya afikirie kuachana na mchezo wa ngumi, na pambano hilo linamjia mara kwa mara kichwani kwake na kujiuliza kwa nini tukio hilo limetokea kwani hakuna anayestahili limtokee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BONDIA AFARIKI DUNIA SIKU NNE TU BAADA YA KIPIGO KIKALI ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top