• HABARI MPYA

  Thursday, October 24, 2019

  KAGERA SUGAR YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 KATIKA MECHI YA LIGI KUU LEO UWANJA WA SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Kagera Sugar leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Ushindi huo unaifanya Kagera Sugar ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi saba, ikijivuta hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu sasa ikilingana na Namungo FC inayoshika nafasi ya pili.
  Hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga na Azam FC, Juma Mwambusi ambayo inabaki na pointi zake nne katika mchezo wa sita.


  Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Kagera Sugar inayofundishwa na Mecky Mexime ilikuwa mbele kwa mabao 3-1 huku ikiwapoteza kabisa wenyeji mbele ya mamia ya mashabiki wao.
  Mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Erick Kyaruzi dakika ya 17 akimalizia pasi ya Abdallah Seseme, Yusuph Mhuli dakika ya 27 akimalizia pasi ya Zawadi Mauya na Frank Ikobela dakika ya 31.
  Bao pekee la Mbeya City lilifungwa na Mohammed Mussa dakika ya 35 akimalizia pasi ya Frank Damas, kabla ya Geofrey Mwashiuya kuifungia Kagera Sugar bao la nne dakika ya 60 akimalizia pasi ya Yusuph Mhilu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 KATIKA MECHI YA LIGI KUU LEO UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top