• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 25, 2019

  WACHEZAJI WATANO WAUMIA BAADA YA BASI LA NDANDA SC KUPATA AJALI NZEGA LEO

  Na Mwandishi Wetu, NZEGA
  WACHEZAJI watano wa Ndanda FC, Aziz Sibo, Paul Maona, Hemed Khoja, Nassor Saleh na Omar Ramadhan wameripotiwa kupata maumivu madogo madogo baada ya basi la timu hiyo kupata ajali wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa safarini kuelekea mkoani Kagera.
  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Barnabas Mwakalukwa, ajali hiyo imetokea baada ya gari ya Ndanda kuligonga basi la abiria la Mtei na kusababisha majeraha kwa wachezaji watano wa Ndanda.
  Ndanda FC wanatarajiwa kuwa wageni wa Kagera Sugar Jumapili Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

  Kwa ujumla Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa Polisi Tanzania Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mechi nyingine za Jumapili ni kati ya Ruvu Shooting na Azam FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Biashara United na Namungo FC Uwanja wa Karume mjini Musoma, Lipuli FC na Coastal Union Uwanja wa Samora mjini Iringa, Mwadui FC na JKT Tanzania Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Singida United dhidi ya Simba SC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. 
  Jumatatu kutakuwa na mechi mbili mjini Mwanza, Uwanja wa Nyamagana Alliance FC dhidi ya Tanzania Prisons na CCM Kirumba ni Mbao FC dhidi ya Mbeya City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WATANO WAUMIA BAADA YA BASI LA NDANDA SC KUPATA AJALI NZEGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top