• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 25, 2019

  MSUVA APIGA BAO LA TATU JADIDA YASHINDA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN 
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva (kushoto) jana ameifungia klabu yake, Difaa Hassan El-Jadida bao la tatu ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Chabab Atlas Khenifra katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Morocco usiku wa jana Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan.
  Msuva ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga alifunga bao hilo dakika ya pili ya muda ziada baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo huo.
  Mabao mengine ya Difaa Hassan El-Jadida yenye mchezaji mwingine Mtanzania, Nickson Kibabage aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar yalifungwa na El Mehdi Karnass dakika ya 49 na Bilal El Magri dakika ya 82.
  Jadida sasa inaungana na Hassania Agadir iliyoitoa Ittihad Tanger, Tihad Casablanca iliyoitoa Ittihad Khemisset na Moghreb Tetouan yenye kiungo Mtanzania, Maka Edward aliyetokea Yanga pia iliyoitoa Rapide Oued Zem na kutinga Nusu Fainali.
  Kikosi cha Difaa Hassan El-Jadidi kilikuwa; Mohamed El Yousfi, Ettayb Boukhriss/Soulaimane Lamrany dk21, Ayoub Benchchaoui, Marouane Hadhoudi, Bakary N’diaye, Youssef Aguerdoum, Abdelfattah Hadraf, Chouaib El Maftoul/Hicham El Massaki dk85, Houssam Amaanan/Khalid Taheri dk74, El Mehdi Karnass, Simon Musva na Bilal El Magri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA APIGA BAO LA TATU JADIDA YASHINDA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top